Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

FAO yalenga kuongeza fedha kwa ajili ya lishe na mabadiliko ya tabianchi

FAO yalenga kuongeza fedha kwa ajili ya lishe na mabadiliko ya tabianchi

Mkurugenzi Mkuu wa shirika la chakula na kilimo duniani, FAO José Graziano da Silva amefungua mkutano wa wiki nzima wa baraza tendaji la shirika hilo akisihi wajumbe walegeze misimamo yao juu ya mpango wa kazi na bajeti ya chombo hicho.

Da Silva amesema bajeti pendekezwa ya zaidi ya dola Bilioni Moja kwa kipindi cha mwaka 2016/2017 ni nyongeza ya asilimia 0.6 ikilinganishwa na bajeti ya sasa na pamoja na kuimarisha lishe..

(Sauti ya Da Silva.)

Zitatumika mahususi kutoa msaada wa nyongeza hususan kwa nchi za visiwa vidogo zinazoendelea ili kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi. Umuhimu wa msaada huu umekuwa bayana zaidi kutokana na madhara yaliyoletwa na kimbunga PAM.”

Da Silva amesema anachowaomba si kutoa tu fedha zao bali ni kuwekeza kwenye chombo chao ili waweze kutekeleza kile wanachowataka wafanye kwa maslahi ya kila mtu hususan maskini, wenye njaa na walio hatarini kukumbwa na madhila.

Bajeti hiyo baada ya kuridhiwa na baraza hilo inatarajiwa kupitishwa na nchi wanachama wa FAO mwezi Juni wakati wa mkutano mkuu.