Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Manusura wa Ebola Sierra Leone wapata pigo upya hata baada ya kupona..

Manusura wa Ebola Sierra Leone wapata pigo upya hata baada ya kupona..

Jamii ya kimataifa kila uchao inahaha siyo tu kusaidia matibabu kwa wagonjwa wa Ebola kwenye nchi zilizokubwa na ugonjwa huo Afrika Magharibi bali pia usaidizi kwa manusura.

Hii ni kwa kuzingatia kuwa watu waliopona ugonjwa huo wanaporejea makwao wanakumbana na madhila makubwa ikiwemo kukataliwa na jamii zao.

Hilo lilinakuwa ni pigo mara mbili kama ilivyo kwa mmojawao huko nchini Sierra Leone kama anavyosimulia Assumpta Massoi kwenye makala hii.