Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban alaani shambulio nchini Libya

Ban alaani shambulio nchini Libya

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban ki-moon amelaani vikali shambulio lililotokea katika hoteli iitwayo Corinthia mjini Tripoli mnamo Januari 27.

Taarifa iliyotolewa na  msemaji wa Katibu Mkuu imesema Bwana Ban ametuma salamu za rambirambi kwa familia za waliopoteza wapendwa wao kufuatia shambulio hilo.

Amesema ugaidi hauna nafasi katika Libya mpya na kwamba hautadhoofisha majadiliano ya kisiasa ambayo yanawezeshwa na Umoja wa Mataifa .

Katibu Mkuu amepongeza ujasiri wa wadau wa Libya katika kushiriki katika majadiliano ya kutafuta suluhu ya amani ya mgogoro.