Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa lalaani ISIL kwa mauaji ya raia wa Japan

Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa lalaani ISIL kwa mauaji ya raia wa Japan

Wajumbe wa baraza la usalama wamelaani vikali mauaji dhidi ya raia wa Japan Haruna Yukawa aliyeuwawa na kundi la waislamu wenye msimamo mkali linalotaka kuweka dola la kiislamu (ISIL.

Taarifa ya baraza hilo ambayo imekiita kitendo hicho cha uwoga na kutaka kuachiliwa mara moja kwa raia mwingine wa Japan Kenji Goto .

Wamesema mauaji hayo ni ukumbusho wa kuongezeka kwa vitisho dhidi ya watu wa Syria wanavyokabiliana navyo kila siku wakiwamo wanahabari

Taarifa ya baraza imeongeza kuwa mauaji hayo yanadhihirisha ukatili unaofanywa na ISIL ambao wanawajibika kwa maelfu ya watu wa Syria na Iraq.

Wajumbe wa baraza la usalama la Umoja wa Mataifa wametaka watekelezaji wa vitendo hivyo wafikishwe katika vyombo vya sheria na kutaka nchi mbalimbali kushirikiana na Japan na mamlaka nyingine katika hili.