Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Twahitaji wataalamu zaidi wa magonjwa na tabia kudhibiti Ebola: Dkt. Nabarro

Twahitaji wataalamu zaidi wa magonjwa na tabia kudhibiti Ebola: Dkt. Nabarro

Visa vya Ebola vinaendelea kupungua kila uchao huko Liberia, Sierra Leone na Guinea, lakini hatupaswi kulegeza jitihada za sasa! Amesema mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu Ebola Dkt. David Nabarro alipohojiwa na Televisheni ya Umoja wa Mataifa mjini New York, akisema shuhuda ni takwimu za sasa ikilinganishwa na mwezi Septemba mwaka jana. Taarifa kamili na Assumpta Massoi.

(Taarifa ya Assumpta)

Nabarro amesema mwezi Septemba visa vipya ya Ebola kwenye nchi hizo tatu zilizoathiriwa zaidi vilikuwa 150 kwa siku lakini sasa ni 50 na hata chini ya hapo kwa siku.

Amesema wanachofanya sasa ni kuhakikisha wanafuatilia wagonjwa na wale waliokutana nao ili visa vipya vitokomezwe kabisa na hatimaye maisha yarejee katika hali ya kawaida.

Kwa mantiki hiyo..

(Sauti ya Dkt. Nabarro)

“Mahitaji muhimu zaidi ni kuwa na watu wenye uzoefu ambao wanafahamu magonjwa na kwa kuwa ugonjwa huu unachochewa na kuenezwa kutokana na tabia za watu hususan wakati wa maradhi au kifo, tunahitaji pia kundi lingine la watu wenye uelewa wa tabia za watu. Hawa wasambazwe kwenye nchi zote zenye maambukizi ili wafuatilie kiwango cha ugonjwa na wafahamu kinachoendelea miongoni mwa jamii na wachukue hatua.”