Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Syria na Mataifa jirani kukumbwa na dhoruba kali ya baridi

Syria na Mataifa jirani kukumbwa na dhoruba kali ya baridi

Wafanyakazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la kuwahudumia wakimbizi, UNHCR wamekuwa wakifanya kazi kila uchao juma hili kuwasaidia mamilioni ya wakimbizi na watu waliofurushwa makwao kukabiliana na dhoruba kali baridi katika maeneo mengi ya Mashariki ya Kati.

Utabiri wa hali ya hewa unaonyesha kuwa hali hiyo ya hewa baridi kali itadumu kwa siku chache huku theluji ikiambatana na upepo mkali unaotarajiwa katika maeneo ya milima.

Licha ya dhoruba kali, ofisi za UNHCR Mashariki ya kati haijapata  ripoti ya uharibifu mkubwa katika jamii za wakimbizi.

Kwa maantiki hiyo, UNHCR imesema kadri hali ya baridi inavyoendelea,  maisha ya wakimbizi yatakuwa magumu.