UNICEF yapambana na utumikishwaji wa watoto miongoni mwa wakulima wa kakao Cote d’Ivoire

UNICEF yapambana na utumikishwaji wa watoto miongoni mwa wakulima wa kakao Cote d’Ivoire

Nchini Cote d’Ivoire, utumikishwaji wa watoto bado ni tatizo, hasa katika jamii za wakulima wanaotegemea kakao. Uzalishaji wa kakao ni kazi ngumu, na wakulima wengi hutumikisha watoto wao. Asilimia 40 ya kakao inayouzwa duniani  inatoka Cote d’Ivoire.Kusini mwa nchi, shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF, limeanzisha kampeni ya kupinga utumikishwaji wa watoto kwa ushirikiano na serikali ya Cote d’Ivoire.

Mradi huo umeanza kuzaa matunda na tayari uandikishwaji shuleni umeimarika. Mwanafunzi Halima, mwenye umri wa miaka 10, ni mfano. Ungana na  Priscilla Lecomte katika makala ifuatayo.