Japo ugumu wa maisha binti lazima aende shule : Samira
Lengo namba 4 la ajenda ya maendeleo andelevu ya Umoja wa Mataifa, linaangazia elimu bora kwa wote. Mashirika ya Umoja wa Mataifa kwa kushirikiana na serikali mbalimbali duniani yamekuwa mstari wa mbele kuhamasha jamii hasa wazazi wahakikishe watoto wote bila kubagua jinsia wanapata elimu .
Katika makala ya leo tunaelekea nchini Somalia ambako tunakutana na Bi. Samira ambaye licha ya yeye kutosomeshwa na baba yake kwa kigezo kwamba yeye ni mtoto wa kike, ameamua kwa nguvu zote kumsomesha binti yake ili aweze kujitegemea katika siku za usoni. Nini kilichotokea kwa Samira baada ya mume wake kufariki ? ungana basi na Patrick newman katika makala hii….. barabara hiyo.