Skip to main content

Wanawake Zanzibar wanajivunia hatua zilizopiga katika usawa wa kijinsia.

Wanawake Zanzibar wanajivunia hatua zilizopiga katika usawa wa kijinsia.

Makala yetu ya wiki leo inazungumzia hatua zilizopigwa katika serikali ya mapinduzi ya Zanzibar kutekeleza malengo ya Beijing.

Miaka kumi na mitano baada ya mkutani wa kimataifa wa wanawake uliofanyika Beinjng, nchi nyingi zimejitahidi kutekeleza malengo ya Beijing na zingine bado zinajikongoja taratibu.Kwa ujumla nchi nyingi zimethibitisha kuwa hakuna lisilowezekana pakiwa na nia na njia.

Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ni moja ya nchi zilizopitia changamoto nyingi katika juhudi za kumkomboa mwanamke, lakini kwa sasa wanjivuna kuwa wamepiga hatua kama alivyonifahamisha waziri wa kazi maendeleo ya vijana wanawake na watoto wa Zanzibar Bi Asha Abdallah Juma.