Skip to main content

Afrika imejitahidi katika usawa wa kijinsia

Afrika imejitahidi katika usawa wa kijinsia

Makala yetu ya wiki leo inazungumzia kumalizika kwa kikao cha 54 cha wanawake hapa makao makuu ya Umoja wa Mataifa New York, ambapo imebainika afrika imepiga hatua katika kumkomboa mwanamke.

Kikao hicho kilichomalizika ijumaa 12 Machi kilijumuisha wawakilishi kutoka nchi mbalimbali duniani, mashirika ya Umoja wa Mataifa na wanaharaktati wa haki za wanawake. Kimetathmini hatua zilizopigwa na nchi mbalimbali katika kumkomboa mwanamke miaka 15 tangu mkutano wa Beijing wa 1995.

Kikao hicho kimehitimishwa kwa kusema pamoja na kwamba bado kuna safari ndefu ya kumkomnoa mwanamke kiuchumi, kisiasa na kijamii, lakini hatua zimepigwa, na chagizo bado inatolewa kwa viongozi kuongeza juhudi kufanikisha malengo.

Bi Getrude Mongela alikuwa katibu mkuu wa mkutano wa Beijing, mwanaharakati wa haki za wanawake na pia Rais mstaafu wa bunge la Afrika. Alitoa mada katika mkutano huu kuhusu maendeleo ya Afrika na amenifahamisha hatua zimepigwa.