Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ni jukumu la Kila Nchi kulinda haki za Wakimbizi: Elliason

Ni jukumu la Kila Nchi kulinda haki za Wakimbizi: Elliason

Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Jan Eliasson amefanya majadiliano leo maafisa wa ngazi za juu wa mashirika yanayohusika na masuala ya uhamiaji na kuangazia biashara haramu ya usafirishaji. Eliasson amekutana na  Kamishna Mkuu wa Shirika la kuhudumia wakimbizi duniani UNHCR Antonio Guterres, Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu kwa ajili ya uhamiaji wa Kimataifa na Maendeleo, Peter Sutherland, na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Kimataifa la Uhamiaji, IOM, William Swing.

Viongozi hao wamejadili uhamiaji wa kimataifa na  mwenendo mpya katika biashara ya haramu ya usafirishaji ikiwa ni pamoja na kutumiwa  kwa meli kubwa ya mizigo na wafanyabiashara katika Bahari ya Meditrenia.

Mtindo huu mpya umesababisha kufariki kwa kwa watu 3,000 katika Bahari ya Meditrenia katika mwaka wa 2014 ikilinganishwa na vifo 700 mwaka wa 2013.

Kuhusu juhudi zinazoendelea za uokozi, haswa la jeshi la Maji la Italia, Nibu Katibu Mkuu amesisitiza jukumu la kila nchi wanachama kuhakikisha ulinzi na haki za binadamu za wahamiaji.