Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Licha ya kufunga ofisi ya Umoja wa Mataifa Burundi tutasaidia uchaguzi : Anyanga

Licha ya kufunga ofisi ya Umoja wa Mataifa Burundi tutasaidia uchaguzi : Anyanga

Licha ya Ofisi ya Umoja wa Mataifa nchini Burundi kufungwa rasmi tarehe 31, disemba, 2014, kufuatia maamuzi ya pamoja ya serikali ya Burundi  na Umoja  huo wa Mataifa, Umoja wa Mataifa utaendelea kusaidia Burundi kimaendeleo na itatuma timu maalum ili kusimamia uchaguzi mkuu unaotakiwa kufanyika mwaka huu.Katika mahojiano na Redio ya Umoja wa Mataifa, Parfait Onanga Anyanga, aliyekuwa mkuu wa ofisi hiyo, amepongeza mafanikio yaliyopatikana nchini katika kuelekea amani na maridhiano na  Kuhusu uchaguzi unaosababisha mivutano ya kisiasa amesema .

“Bado tuko kwenye nchi inayorejelea maisha ya kawaida baada ya vita, ambapo utengamano umekuwa sababu ya msingi ya mzozo. Na labda demokrasia bado ni kitu kipya nchini Burundi, hata kama napaswa kusema kwamba nchi imefanikiwa kuandaa uchaguzi mbili mwaka 2005 na mwaka 2010. Changamoto hizo, kwa maoni yangu, zinaweza kufunguliwa. Ndio kitu nachoshuhudia. Ndio maana, kama wanaweza kutekeleza mpango wa kazi ulioandaliwa, naamini kwamba Burundi inaweza kuandaa uchaguzi bora mwaka 2015”