Mkutano wa utalii duniani kufanyika Haiti

29 Disemba 2014

Haiti inatarajiwa kuwa mwenyeji wa mkutano wa kimataifa juu ya utalii ambao umepangwa kufanyika katika mjii mkuu wa Port au Prince ikiwaleta pamoja wataalamu mbalimbali.

Mkutano huo ambao umendaliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na Utalii unafanyika nchini humo kwa mara ya kwanza na mwamba unatazamiwa kutoa fursa kwa nchi hiyo kuonyesha vitega uchumi vyake na maendeleo kwa ujumla.

Mkutano huo umepangwa kufanyika Mei 19 -22 mwakani. Kwa hivi sasa Wizara ya Utalii nchini Haiti imekuwa ikichukua hatua muhimu kukusa sekta ya utalii kwa ajili ya kukuza ajira na kukusanya fedha za kigeni.

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter