Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baraza la Usalama lalaani mashambulizi ya kigaidi Peshawar

Baraza la usalama. (Picha-Maktaba)

Baraza la Usalama lalaani mashambulizi ya kigaidi Peshawar

Wajumbe wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa wamelaani vikali mashambulizi ya kigaidi yaliyofanywa katika shule moja mjini Peshawar nchini Pakistan na kusabisha mauaji ya zaidi ya raia 140 wakiwemo wanafunzi 132. Taarifa kamili na Joseph Msami.

(Taarifa ya Msami)

Katika tamko lao, wajumbe wa baraza wameita tukio hilo kuwa ni la kigaidi na kuongeza kuwa uhalifu wa namna hiyo haukubaliki kwa namna yoyote ile. Kundi la kigaidi la Taliban limedai kuhusika katika shambulizi hilo ambalo pia limesababisha mamia ya watu kujeruhiwa.

Baraza hilo limetuma salamu za rambirambi kwa familia na ndugu waliopoteza maisha kwenye shambulizi hilo na kuelezea kuunga mkono juhudi zinazochukuliwa na serikali kuwalinda wanafunzi na maeneo mengine muhimu.