Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Peru imepiga hatua dhadhiri katika MDGs: Ban

Hap ni katika ikulu ya rais wa Peru wakati alipokea Katibu MKuu wa UM Ban Ki-moon(Picha ya Mark Garten)

Peru imepiga hatua dhadhiri katika MDGs: Ban

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema mafanikio yaliyofikiwa na Peru katika utekelezaji wa malengo ya maendeleo ya milenia, MDGs, yanaisogeza  dunia kukaribia kutimiza malengo hayo.

Akihutubia baraza la Kongresi la nchi hiyo Bwana Ban amesema Peru imefanikiwa kutafsiri ukuaji wa kiuchumi katika kupunguza umasikini kwa zaidi ya asilimia 50 huku akiyataja mafanikio mengine kuwa ni elimu kwa wote .

Amesema Peru imefanikiwa kwa kiasi kikubwa kupunguza vifo vya watoto wachanga, utapiamlo na kupunguza hatari ya vifo vya wanawake wajawazito.

Kadhalika Bwana Ban amesifu mafaniko mengine yaliyofikiwa akisema idadi kubwa ya raia nchini Peru sasa wanapata maji na huduma za kujisafi

Katika hatua nyingine Katibu Mkuu ameipongeza Peru ambayo imekuwa mwenyeji wa mkutano wa 20 wa mabadiliko ya tabianchi COP 20 kuwa imepiga hatua katika usawa wa kijinsia akitaja mfano wa baraza hilo la Kongress kuongozwa na mwanamke.