Sampuli za damu zasafirishwa kwa helkopta Liberia : UNMEER

26 Novemba 2014

Wakati juhudi za kupambana na Ebola zikiendelea kwa mara ya kwanza sampuli za damu zimesafirishwa nchini Siera Leone kwa kutumia helikopta kutoka Kumala hadi  Bo ikiwa ni sehemu ya mpango wa kusafirisha mara tatu sampuli hizo kwa wiki kutoka vijijini kwa wiki nane zijazo.

Taarifa ya ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kushughulikia dharura ya Ebola UNMEER inasema kuwa ujumbe huo kwa kushirikiana na kituo cha udhibiti na kuzuia  magonjwa  CDC kutekeleza zoezi hilo nchini Liberia ambapo shirika la mango wa chakula duniani WFP limeomba ndege mbili. Mpango huu unalenga Liberia kuwa na helkopta mbili na Guinea moja.

Wakati huohuo wafanyakazi wa maziko mjini Kanema  nchini Liberia wametelekeza miili hadharani kufuatia mgomo unaoendelea. Miili 15 inadaiwa kutelekezwa katika hospitali ya mji huo pamoja na lango kuu la kuingilia. Wafanyakazi hao wameachishwa kazi kwa vitendo hivyo ambavyo UNMEER imeviita vya kinyama.

Katika hatua nyingine ofisi ya UNMEER nchini Mali imeanza rasmi kazi zake za kukabiliana na kirusi cha Ebola nchini humo November 20 mwaka huu baada ya kuagizawa hivi karibuni na Umoja wa Mataifa kufungua ofizi hizo katika nchi ambayo imetajwa kuwa na visa kadhaa vya Ebola

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud