Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban asihi ushirikiano katika serikali ya mpito Burkina Faso

Bango la kuhamasiha ujumbe wa amani nchini Burkina Faso.(Picha ya IRIN/Chris Simpson)

Ban asihi ushirikiano katika serikali ya mpito Burkina Faso

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon, ameelezea ufahamu wake kuhusu uteuzi wa wanachama 26 wa serikali ya mpito hapo jana, na kukutana kwa Baraza la mawaziri leo kwa mara ya kwanza nchini Burkina Faso. Taarifa ya msemaji wake imesema Bwana Ban anatazamia uteuzi wa wanachama wa Baraza la Kitaifa la Mpito.

Katibu Mkuu ametoa wito kwa viongozi wote wa mpito kushirikiana kwa njia ya amani ili kuhakikisha kuwa ndoto za watu wa Burkina Faso zinatimia. Stephane Dujarric ni msemaji wa Katibu Mkuu

Ametoa wito pia kwa wadau wote wa kitaifa kushughulikia masuala yoyote ya utata kupitia mazungumzo, ili kuhakikisha kipindi tulivu cha mpito, hadi uchaguzi utakapofanyika Novemba mwakani.”

Katibu Mkuu pia amesema Umoja wa Mataifa utaendelea kufanya kazi kwa karibu na Muungano wa Afrika, AU, Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Afrika Magharibi, ECOWAS na wadau wengine wa kimataifa katika kuunga mkono serikai ya mpito ya taifa hilo.