Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mazungumzo ya Darfur yafanyika Addis Ababa.

Walinda amani walioko Darfur wakiwa katika moja ya doria zao. (Picha:Albert González Farran, UNAMID)

Mazungumzo ya Darfur yafanyika Addis Ababa.

Kaimu mpataninishi wa mzozo wa Darfur nchini Sudan kutoka Umoja wa Afika na Umoja wa Mataifa Abiodun Bashua ameshiriki katika mazungumzo ambayo yamewakutanisha makundi ya waasi na serikali ya Sudan.

Mazungumzo hayo yaliyofanyika Addis Ababa, Ethiopia yamejumuisha makundi ambayo yalikuwa bado hajasaini makubaliano ya amani ya Darfur.

Akizungumza kwenye mazungumzo hayo Mwenyekiti wa kikao hicho rais mstaafu wa Afrika Kusini Thabo Mbeki alipongeza hatua ya kufanyika majadiliano hayo akisema kuwa yanatoa ishara yenye kutia matumaini.