Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kampeni za uchaguzi wa maseneta Liberia kuanza kesho

Juhudi za kutoa elimu kwa watoto kwa ajili ya kukabiliana na Ebola nchini Liberia.(c) UNICEF / Liberia / 2014 / Carolyn Marie Kindelan

Kampeni za uchaguzi wa maseneta Liberia kuanza kesho

Nchini Liberia, Tume ya Taifa ya uchaguzi imesema kampeni rasmi za uchaguzi maalum wa maseneta zitaanza rasmi kesho tarehe 20 licha ya mlipuko wa Ebola.

Tume hiyo hata hivyo imetaka wagombea na wafuasi wao kuzingatia kanuni zote za afya ya umma zilizowekwa na serikali ili kuzuia kuenea kwa ugonjwa wa Ebola wakati wa kampeni hizo. Awali uchaguzi huo ulikuwa ufanyike mwezi Oktoba.

Katika hatua nyingine Taarifa iliyotolewa na ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kushughulikia dharura ya Ebola, UNMEER imesema India imemuweka chini ya karantini raia wake mmoja aliyerejea nchini humo kutoka Liberia baada ya sampuli za uchunguzi kubaini kuwa bado ana masalia ya kirusi hicho kwenye mwili wake.

Wizara ya afya ya India imesema ataendelea na karantini hiyo hadi pale kirusi hicho kitakapoondoka kabisa mwilini mwake.