Machafuko Iraq yasababisha madhila kwa raia: OCHA

17 Novemba 2014

Machafuko yanayoendelea nchini Iraq yamesabaabisha zaidi ya watu milioni moja na laki tisa kupoteza na kuhamia katika sehemu tofauti . Taarifa zaidi na Joseph Msami

(TAARIFA YA MSAMI)

Kwa mujibu wa ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kuratibu misaaada ya kibinadamu OCHA, mapigano yanayoendelea hususani vuguvugu la kundi la dola ya kiisilamu  ISIL limesabisha mtawanyiko wa watu likisema mathalani wiki iliyopita pekee kuliripotiwa kiwango kikubwa cha raia kupoteza makazi katika wilaya iitwayo

Salah al-Din karibu na Tikrit

OCHA imesema ISIL na makundi yake yalitoa amri ya watu kutoka katika makazi yao kwa kutoa saa 24 kwa baadhi ya makabila hali iliyochochea zaidi ukosefu wa makazi.  Hali ya sintofahamu sasa aimetanda nchi nzima ambapo hakuna utulivu.

Shirika hilo limeonya kuongezeka kwa idadi ya raia wanaopoteza makazi nchini humo.

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud