Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tanzania iko kwenye mwelekeo sahihi kudhibiti Numonia:UNICEF

Mtoto akipewa chanjo. Photo © UNICEF Burundi/Krzysiek

Tanzania iko kwenye mwelekeo sahihi kudhibiti Numonia:UNICEF

Ikiwa leo ni siku ya kimataifa ya kudhibiti ugonjwa wa Numonia, Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF limesema muongo mmoja uliopita umeshuhudia kupungua kwa kiasi kikubwa kwa vifo vya watoto vitokanavyo na ugonjwa huo ujulikanao pia kama vichomi.

Taarifa ya UNICEF inasema vifo miongoni mwa watoto wenye umri wa chini ya miaka mitano vimepungua kwa asilimia 44 ikilinganishwa na idadi ya mwaka 2000.

Nchini Tanzania hali ya Numonia nayo inapungua ambapo Dkt. Thomas Lyimo kutoka Idara ya Afya na Lishe ya UNICEF anataja sababu ni pamoja na utekelezaji wa mpango wa udhibiti wa magonjwa ya watoto kwa uwiano.

 (Sauti ya Dkt. Lyimo)

Kuhusu changamoto za kuhifadhi mafanikio hayo, Dkt. Lyimo amesema jamii inapaswa kuwa macho zaidi.

(Sauti ya Dkt, Lyimo)

Mahojiano kamili na Dkt. Lyimo yatapatikana kwenye tovuti yetu.