Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mashauriano yarejeshe utawala wa kikatiba Burkina Faso:IPU

Nembo ya IPU

Mashauriano yarejeshe utawala wa kikatiba Burkina Faso:IPU

Muungano wa mabunge duniani, IPU umeshutumu ripoti za kuvunjwa kwa bunge nchini Burkina Faso ukitaka pande zinazokinzana kushauriana ili utawala wa kikatiba urejee mapema iwezekanavyo.

Rais wa IPU Saber Chowdhury amesema kwa mara nyingine tena kitendo cha bunge kuvamiwa na kushambuliwa kinaonyesha jinsi bunge linavyokuwa mhanga wa udhaifu wa wanasiasa kufikia makubaliano.

Ameelezea wanachukizwa na ghasia zinazoendelea na kwamba utawala wa kikatiba ndio suluhisho la kudumu la mustakhbali wa amani na tulivu nchini Burkina Faso.

Bwana Chowdhury amesema wanafuatia kwa umakini hali inavyoendelea.