Ban awapongeza watu wa Tunisia kufuatia uchaguzi wa wabunge

27 Oktoba 2014

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon, amewapongeza raia wa Tunisia kwa uchaguzi wa ubunge uliofanyika jana Jumapili Oktoba 26, 2014.

Kama alivyosema katika ziara yake hivi karibuni nchini Tunisia, uchaguzi huo ni hatua muhimu kwa mustakhbali wa taifa hilo, na unaweka msingi thabiti kwa demokrasia.

Hata hivyo, Ban amesema ingawa wakati huu unaleta matumaini makubwa, bado kuna majukumu muhimu mbele kwa serikali ijayo. Amekariri kuwa Umoja wa Mataifa u tayari kuunga mkono Tunisia katika kutekeleza majukumu hayo.

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter