UM waipongeza Sudan kwa kuwapokea wakimbizi wa Sudan Kusini

23 Oktoba 2014

Mjumbe wa Katibu Mkuu kuhusu masuala ya kibinadamu, Abdullah al Matouq na Kamishna Mkuu wa Shirika la Kuwahudumia Wakimbizi, António Guterres wameipongeza serikali ya Sudan kwa kuwakaribisha wakimbizi wa Sudan Kusini kwa ukarimu.

Maafisa hao wa Umoja wa Mataifa wametoa sifa hizo mara tu baada ya kurejea kutoka kwa ziarayaokatika jimbo la White Nile nchiniSudan, ambako zaidi ya wakimbizi 50,000 wa Sudan Kusini wanaishi sasa hivi katika vituo vinne.

Wakiwa huko, walitembelea pia eneo la mpakani la Joda, ambako wengi wa wakimbizi wa Sudan Kusini wamekuwa wakiuvikia kuingiaSudan, na pia kutembelea kituo cha wakimbizi cha Al Alagaya, ambacho kinawapa hifadhi wakimbizi 8,000. Waliweza kujionea moja kwa moja hali ya maisha ya wakimbizi wanaokimbia machafuko na ukatili Sudan Kusini wakitafuta usalama nchini Sudan.

Wamesema kuwa wakimbizi hao wamo katika hali mbaya mno, kwani wamepotza nyumba zao, vitega riziki na jamaa zao, na hivyo wameishukuru serikali yaSudanna watu wake kwa ukarimu wanaoendelea kuwaonyesha raia hao wa Sudan Kusini.

Zaidi ya wakimbizi 100,000 wamewasiliSudantangu kuanza kwa mapigano Sudan Kusini katikati mwa mwezi Disemba mwaka jana, na takriban wakimbizi 1,000 wanaendelea kuwasili kila wiki, na hivyo kuifanya hali ya kibinadamu nchinSudakuwa mbaya zaidi.

 

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa UNGA76 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter