Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban alaani kufukuzwa kwa afisa wa haki za binadamu DRC

UN Photo.
Stephane Dujarric.

Ban alaani kufukuzwa kwa afisa wa haki za binadamu DRC

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amelaani uamuzi wa serikali ya Jamhuri ya kidemokrasi ya Congo DRC wa kumpatia afisa wake mwandamizi saa 48 kuondoka nchini humo huku maafisa wengine wakikumbwa na vitisho.

Akiongea na waandishi wa habari mjini New York msemaji wa Katibu Mkuu Stephan Dujarric  amesema Katibu Mkuu amesisitiza kuwa watu wa DRC wameteseka kwa muda mrefu kutokana na kudorora kwa haki nchini humo na ofisi hiyo ilikuwa na lengo la kuimarisha haki na uwajibikaji kwa watu wa DRC na kuitaka serikali kufikiria tena juu ya umauzi huo.

Ban amesema kwa mujibu wa mkataba wa Umoja wa Mataifa  , wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa wanaojihusiha na masuala ya haki za binadamu hawapaswi kuwekewa vikwazo  wala kutishiwa kwa kufanya kazi yao.

Ametaka baraza la usalama kufikiria madhara kama hayo pale wafanyakazi wanapokumbana na vikwazo kama hivyo na kulitaka barazahilokufikiria hatua za kuchukua.

 Afisa aliyefukuzwa Scott Campbell alikuwa Mkurugenzi wa ofisi ya pamoja ya Umoja wa Mataifa kuhusu haki za binadamu.