Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkuu wa MONUSCO aonyesha mshikamano na familia za waliouawa Beni

Martin Kobler, Mkuu wa MONUSCO.(Picha ya UN/Rick Bajornas)

Mkuu wa MONUSCO aonyesha mshikamano na familia za waliouawa Beni

Martin Kobler, Mkuu wa Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, MONUSCO, amekwenda kutoa heshima zake kwa wahanga wa shambulizi la Oktoba 15 usiku katika mitaa ya Ngadi na Kadu karibu na mji wa Beni, jimbo la Kivu Kaskazini.

Wakati wa hafla hiyo, Bwana Kobler alikutana na familia za wahanga hao wa mashambulizi ya kundi la waasi wa ADF, akisema kwamba amekwenda Ben kwa minajili ya kuonyesha mshikamano wake na kutoa rambi rambi zake kwa familia hizo.

Amelaani tena vikali mauaji ya kinyama yanayotekelezwa na ADF, akiongeza kuwa bila shaka watawajibishwa kwa uhalifu huo usioweza kukubalika. Kobler alikuwa ameandamana na Gavana wa Kivu-Kaskazini, Julien Paluku na Naibu Kamanda wa kikosi cha MONUSCO, Jean Baillaud.