Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNHCR, Uganda waanza kurejesha wakimbizi wa DRC

Msafara wa wakimbizi hao wakipanda basi.(Picha ya UM/Idhaa ya kiswahili/John Kibego)

UNHCR, Uganda waanza kurejesha wakimbizi wa DRC

Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR) na serikali yaUganda, wameanza kuwarudisha nyumbani kwa hiari wakimbizi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC).

Hatua hii imekuja baada ya mamia ya wakimbizi kurudi kwao wakitumia njia hatarishi na kusababishaa kuzama ziwani kwa zaidi ya wakimbizi 100 mapema mwaka huu .

Tarifa kamili na John Kibego wa redio washirika ya Spice FM nchini humo.

(Tarifa ya John Kibego)