Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNMEER yasisitiza Ebola haiambukizwi kwa njia ya hewa:

Watoa huduma ya afya, kando na kuvaa mavazi ya kujikinga dhidi ya ebola wanahitajika kusafisha mahali ambapo amekuwa mgonjwa wa ebola.WHO/Christina Banluta

UNMEER yasisitiza Ebola haiambukizwi kwa njia ya hewa:

Ujumbe wa dharura wa Umoja wa mataifa kuhusu Ebola, UNMEER, umetoa taarifa yake inayosisitiza kuwa hakuna uthibitisho wowote hivi sasa juu ya uwezekano wa kirusi cha ugonjwa huo kubadilika na kuweza kuambukizwa kwa njia ya hewa.

Taarifa hiyo imesema kuna hofu juu ya mlipuko huo huko Liberia, Guinea na Sierra Leone ambako kila siku watu wengi zaidi wanaambukizwa na wengine wanafariki dunia kwa sababu hawapati tiba wanayohitaji.

Kwa mantiki hiyo UNMEER imesema jitihada zinapaswa kuelekezwa kwenye mahitaji yanayotakiwa ili kutoa huduma stahili kwenye maeneo yenye mlipuko na kuepusha mambukizi.

Kupitia taarifa hiyo, Shirika la Afya duniani WHO limesisitiza kuwa Ebola inaambukizwa kupitia majimaji ya mgonjwa na vifaa alivyotumia mathalani matandiko, mashuka na hivyo kinachotakiwa sasa ni kila mtu kuepuka kupata majimaji hayo.