Mapigano Iraq yazidi kuchukua uhai wa watu:UNAMI

1 Oktoba 2014

Ofisi ya ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Iraq, UNAMI imetoa takwimu za vifo na majeruhi kutokana na mapigano yanayoendelea nchini humo ambapo raia na polisi wameendelea kuwa wahanga wa zahma hiyo. Taarifa zaidi na Assumpta Massoi.

(Taarifa ya Assumpta)

Kwa mujibu wa takwimu zilitolewa na UNAMI, takriban wairaq 1119 waliuawa ilhali wengine 1964 walijeruhiwa kwenye vitendo vya ugaidi na mapigano kwa mwezi uliopita wa Septemba.

Taarifa hiyo imesema kati ya vifo hivyo raia ni 854 wakiwemo polisi kanzu ikieleza kuwa takwimu hizo hazijumuishi jimbo la Anbar kwa kuwa UNAMI imeshindwa baadhi ya matukio.

UNAMI inasema mji mkuu Baghdad ndiyo uliopata wahanga wengi wa vitendo hivyo ikifuatia na Salahadin , Kirkuk na Diyala.

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter