Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Watu wa asili wapaza sauti kwa pamoja katika mkutano New York

Anne Samante, mshiriki mkutano wa watu wa asili.(Picha ya UN/Grace Kaneiya)

Watu wa asili wapaza sauti kwa pamoja katika mkutano New York

Wakati mkutano wa watu wa asili umemalizika kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York washiriki wa mkutano huo wana ujumbe na maombi rasmi ambayo wanataka serikali zao zishughulikie.

Mkutano huo ambao ulujumuisha watu wa asili wa mataifa mbali mbali kote ulimwenguni ulifanyika hapa ukiwa na lengo la kupazia sauti matakwa ya jamii hii ambayo kwa muda mrefu imekuwa ikitengwa katika maendelo na uamuzi muhimu katika jamii.

Katika makala ifuatayo Joseph Msami alizungumza na baadhi yao kandoni mwa mkutano huo, ungana naye.