Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wacheza filamu na wasomi wajadili uelewa wa biashara ya utumwa

LOUIS GOSSETT, aliyecheza filamu ya Roots kama Fiddler. Picha: Joshua Mmali/Radio ya UM

Wacheza filamu na wasomi wajadili uelewa wa biashara ya utumwa

Wiki iliyopita mjini New York, ziliandaliwa shughuli mbili kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa, kama sehemu ya kuadhimisha miaka 20 ya mradi wa kumbukumbu ya barabara ya biashara ya utumwa.

Kwanza, ulifanyika mjadala kuhusu jinsi utumwa unavyoonyeshwa kwenye filamu, na kisha kukawa na mdahalo kuhusu kufundisha wanafunzi shuleni na watu kujielimisha kuhusu biashara ya utumwa ya Atlantiki. Mwenzetu Joshua Mmali alikwenda kufuatilia shughuli hizo