Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mahitaji ya madini ya urani itaendelea kupanda: IAEA

watalaam wa IAEA wakipima maji ya bahari, karibu ya Fukushima. @IAEA/David Osborn

Mahitaji ya madini ya urani itaendelea kupanda: IAEA

Mahitaji ya madini ya urani, malighafi inayotumiwa kama nishati ya vituo vya nguvu za nyuklia duniani kote, itaendelea kupanda katika siku za karibuni, licha ya kushuka kwa bei za soko tangu ajali ya kituo cha umeme cha nyuklia cha Fukushima Daiichi nchini Japan Machi 2011, sambamba na mahitaji ya chini ya umeme kwa sababu ya mtikisiko wa uchumi duniani.

Haya ni miongoni mwa matokeo ya msingi ya riporti mahususi iliyotolewa leo na Shirika la Kimataifa la Nguvu za Atomiki pamoja na Kitengo cha nishati ya Nyuklia cha Shirika la Ushirikiano wa Kiuchumi na Maendeleo, OECD.

Ripoti hiyo ijulikanyo kama Red Book, imeelezea kuongezeka kwa urani, utafutaji na pia uzalishaji .

Tangu kuchapishwa kwa ripoti ya mwaka wa 2012, asilimia saba ya raslimalia ya urani imetambuliwa na kwa hivyo kuongeza karibu miaka 10 ya rasilimali zilizopo.

Duniani, uzalishaji wa urani kati ya mwaka wa 2010 na 2012, uliongezeka japo kwa kiasi kidogo kuliko kipindi cha miaka miwili ya awali.