Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNAMID yasema kujumuishwa kwa waasi wa zamani wa JEM-SUDAN ni dalili za amani Darfur

Mkuu wa kikosi cha UNAMID Luteni Jenerali Paul Mella. (Picha:Sojoud Elgarrai UNAMID).

UNAMID yasema kujumuishwa kwa waasi wa zamani wa JEM-SUDAN ni dalili za amani Darfur

Wiki hii imekuwa njema kwa mustakabali wa jimbo la Darfur ambalo kwa muda mrefu limeshuhudia mgogoro wa wenyewe kwa wenyewe. Hizi ni taarifa za kujumuishwa kwa waasi  wa zamani wa kikundi cha JEM-SUDAN kwenye jeshi la kitaifa nchini Sudan kufuatia hatua ya kikundi hicho kutia saini makubaliano ya Doha kuhusu amani Darfur.

Kwa mujibu wa Ujumbe wa pamoja wa Umoja wa Mataifa na Muungano wa Afrika huko Darfur, UNAMID umesema hilo ni kundi la kwanza kutoka takribani askari 2700 ambao hatimaye watajiunga na jeshi la kawaida.

Kufuatia hatua hiyo Joseph Msami wa idhaa hii amezungumza na  Mkuu wa vikosi vya UNAMID Luteni Jenerali Paul Mella na kwanza amenza kumuuliza wamepokeaje hatua hiyo.

(SAUTI MAHOJIANO)