Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Haki za wazee zamulikwa kwenye mkutano wa New York

UN Photo / Grunzweig
Wachezaji wawili wakifurahia mchezo wa chesi katika jiji la New York. Picha:

Haki za wazee zamulikwa kwenye mkutano wa New York

Kikao cha tano cha kamati ya inayoshughulikia masuala ya wazee kinamalizika leo hapa kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York, kikimulika masuala ya haki za binadamu za watu wazee. Taarifa kamili na John Ronoh

Kamati hiyo inayoshughulikia haki za wazee iliundwa kufuatia azimio namba 65/182 la Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa mnamo Disemba mwaka 2010. Katika kikao hiki cha tano kilichoanza mnamo tarehe 30 Julai, kamati hiyo imekuwa ikizingatia mkakati wa kimataifa uliopo kuhusu haki za binadamu za wazee, na kujaribu kutambua upungufu au dosari iliyopo katika mkakati huo na njia bora ya kukabiliana nayo.

Kikao cha leo pia kimemkaribisha mwenyekiti mpya wa Kamati hiyo, Bi Rosita Kornfeld-Matte wa Chile, ambaye aliteuliwa na Baraza la Haki za Binadamu mwezi Mei kama Mtaalam Huru kuhusu haki za binadamu za wazee. Bi Matte amesema bado kuna kazi nyingi ya kufanya kuhusu haki za wazee

Matte CLIP

Tungependa kufanya kazi katika ngazi ya kimataifa,

“Ningependa kusema kuwa tutafanya kila tuwezalo kuona kuwa tunapata njia na suluhu kwa dosari zilizopo na kuhakikisha kuwa tumefikia maafikiano kuhusu jinsi ya kulinda haki za wazee. Ningependa haki za wanawake, walemavu na watoto zilindwe, lakini wazee pia ni lazima walindwe”

Mjadala wa leo umejikita zaidi katika kukabiliana na ukatili dhidi ya wazee.