Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wafugaji wakimbizi wasaidiwa na Fao Waziristan Kazkazini nchini Pakistan

Picha ya FAO

Wafugaji wakimbizi wasaidiwa na Fao Waziristan Kazkazini nchini Pakistan

Mapigano yanayoendelea kwenye maeneo ya milima ya Waziristan Kazkazini, nchini Pakistan, yamesababisha takriban watu 800,000 kukimbia makwao.

Shirika la Chakula na Kilimo FAO linakadiria kwamba asilimia 70 ya watu wamekimbia na mifugo wao, na kwa hivyo hawakuweza kupanda magari au basi, na wakalazimika kutembea kwa mwendo mrefu. Mifugo wengi, hususan ng'ombe, wamefariki wakati wa safari hiyo.

Taarifa zinasema kwamba katika kambi za wakimbizi, mifugo waliosalia wamekonda na kudhoofika sana. Shirika la FAO limeamua kutoa misaada kwa mifugo hao ili kuzuia kuhakikisha kwamba wakimbizi hawapotezi mali yao.

Hatua ya kwanza iliyochukuliwa ni kusambaza chanjo 100,000 ili kukinga mifugo dhidi ya ugonjwa wa PPR ambao ni aina ya kirusi kinachoambukiza sana, huku FAO ikijiandaa kutoa msaada wa vyakula na maji.