Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Dola milioni 982 zahitajika kutimiza mahitaji ya kibinadamu Sudan

Watoto hawa wacheza katika kituo cha jamii kilichojengwa na UNAMID katika kambi ya wakimbizi wa ndani , Khor Abeche, kusini Darfur (Picha/UM/Albert González Farran/NICA)

Dola milioni 982 zahitajika kutimiza mahitaji ya kibinadamu Sudan

Kuwepo kwa ongezeko kubwa la mahitaji ya kibinadamu nchini Sudan katika kipindi cha miezi sita ya mwaka huu kumelazimu kupitiwa upya mpango wa misaada ya dharura iliyowekwa hapo awali. Taarifa kamili na John Ronoh.

(Taarifa ya John Ronoh)

Mashirika ya misaada kwa ajili ya Sudan yanasema kuwa kiasi cha dola za Marekani milioni 982 kinahitajika ili kuyakwamua maisha ya watu zaidi ya milioni 6.9 ambao wanakabiliwa na matatizo mbalimbali.

Idadi hiyo ni sawa na asilimia 20 ya wakazi wote wa Sudan wanaohitaji msaada wa dharura na kwamba misaada hiyo inayohitajika ni pamoja na sehemu za kuishi vyakula, madawa na maji.

Ripoti zinaonyesha kuwa katika kipindi cha nusu mwaka, kumeshuhudiwa idadi kubwa ya watu wakipoteza makaziyao katika eneo la Darfur na hali hiyo inaelezwa kuwa ni ya kipekee kwa mwaka huu 2014.

Mzozo unaofukuta huko Sudan Kusini umesababisha mamia ya raia kuyahama makaziyaona kuingia nchini Sudan kwa ajili ya kupata hifadhi.

Inakadiriwa kuwa zaidi ya watu 85,000 wameyahama makaziyaokutokana na machafuko hayo.