Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Madawa ya kulevya yanaathiri ukuaji wa uchumi na maendeleo

Madawa ya kulevya yanaathiri ukuaji wa uchumi na maendeleo

Biashara haramu ya madawa na mashirika ya uhalifu yanaathiri maisha ya watu na jamii kwa ujumla, amesema katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon  katika ujumbe wake maalum alioutuma kwenye mkutano wa viongozi kuhusu tatizo la madawa ya kulevya duniani.  Mkutano huo ulioandaliwa na Baraza la Uchumi na Kijamii la Umoja wa Mataifa, ECOSOC, ulikuwa na lengo la kuangalia jinsi gani tatizo la madawa ya kulevya linaathiri malengo ya maendelo ya milinea na ajenda ya baada ya 2015.

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon hapo amesema:

“Madawa ya kulevya na uhalifu yanayakumba mataifa ambayo tayari ni dhaifu, zinadhoofisha mfumo wa sheria na mamlaka za serikali, na zinaharibu jamii. Shughuli za maendeleo zinaweza kukabiliana na shida hizo”

Hapo amewaomba nchi wanachama zijadili ili kupata suluhu endelevu ambazo zitakuwa sambamba na ajenda ya maendeleo baada ya 2015.  Alipozungumza wakati wa uzinduzi wa mkutano huo, raisi wa ECOSOC, Martin Sajdik, amesema kuna jinsi nne za kupambana na janga la madawa ya kulevya. Kwanza sekta ya afya, akisisitiza umuhimu wa utafiti katika kuimarisha matibabu na kinga.

Pili, uchumi mbadala, yaani kuwashawishi wakulima kulima mazao mbadala ya yale ambayo yanatumika kwa kutengeneza madawa ya kulevya. Amesema pia ni muhimu kuheshimu haki za binadamu katika vita dhidi ya madawa ya kulevya, na mwishowe, ubia wa kimatifa upewe kipaumbele ili kuongeza nguvu kwenye vita hivyo.

Mkutano mkubwa kuhusu madawa ya kulevya unatakiwa kufanyika mwaka 2016.