Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baraza la Usalama lamulika hali tete ya Mashariki ya Kati

Baraza la Usalama

Baraza la Usalama lamulika hali tete ya Mashariki ya Kati

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, leo limekutana kujadili hali Mashariki ya Kati na suala la Palestina, likimulika zaidi hali ya machafuko ambayo sasa yametanda eneo la Gaza. Taarifa kamili na Amina Hassan

(Taarifa ya Amina)

Wakati wa kikao cha leo, Baraza la Usalama limemsikiliza kwanza Katibu Mkuu Ban Ki-moon, ambaye amesema kwamba hivi sasa kuna hatari ya kuibuka machafuko zaidiIsraelnaGaza, ambayo yataweza kuzuiwa tu ikiwa kundi la Hamas litakomesha urushaji makombora.

Ban ambaye amezungumza pia kuhusu mauaji ya vijana wa Kipalestina na Waisrael hivi karibuni, amesema kuwa wakati huu kuna haja ya dharura ya kutafuta suluhu la pamoja, ili utulivu urejeshwe na kusitishwe mapigano.

“Kwa mara nyingine tena, raia ndio wanaoathirika na kuendelea kwa mzozo huu. Ninalojali zaidi ni usalama na maslahi ya raia wote, bila kujali wapo wapi. Inanitia uchungu, na inapaswa kututia sote uchungu, kuona tena hali hii ambayo inatukumbusha kuhusu vita vya Gaza vya hivi karibuni zaidi.”

Ban amelaani mashambulizi ya roketi dhidi yaIsraelkutokaGaza, huku akisema kuwa matumizi ya nguvu kupindukia na kuhatarisha maisha ya raia hakuwezi kukubalika.

“Haikubaliki kwa raia wa pande zote kuishi daima katika hofu. Pande zote, yakiwemo makundi ya Kipalestina yenye silaha ni lazima yaheshimu sheria ya kimataifa ya kibinadamu.”