Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kuwaelimisha wasichana ndio ufunguo wa maendeleo endelevu

Wanafunzi wa kike Tanzania @UNICEF Tanzania / Holt 2014

Kuwaelimisha wasichana ndio ufunguo wa maendeleo endelevu

Mkutano wa kutoa ahadi za kusaidia utoaji elimu kote duniani umechangisha dola bilioni 28.5 kutoka kwa wafadhili na nchi zinazoendelea.

Mkutano huo wa Ubia wa Kimataifa kwa ajili ya Elimu au GPE ulifanyika mjini Brussels, Ubeljiji kati ya tarehe 25 na 26 Juni, ukilenga kuchangisha fedha zaidi za kusaidia upatikanaji elimu. Fedha hizo za ziada zitasaidia kuongeza rasilmali za elimu kwa makumi ya mamilioni ya watoto kutoka nchi 60 zinazoendelea.

Bi Julia Gillard, mwenyekiti wa halmashauri ya GPE na waziri wa zamani wa Australia alizungumza na Mia Lobel wa UNICEF kuhusu ni kwa nini mfumo wa ubia wa GPE unafanikiwa.

“Nadhani GPE inachoweza kutoa, ambacho ni cha aina yake, ni mfumo huu wa ubia- sisi ndilo kundi pekee linaloleta pamoja wa nchi wafadhili, nchi zinazoendelea, mashirika ya umma, na tunafanya hivyo siyo tu kwenye ngazi ya bodi, bali tunafanya kazi katika nchi zinazoendelea, ili ziweke mpango wa elimu kamilifu ambao kila mtu anafurahia na kila mtu anaunga mkono”