Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Australia kuwafukuza wahamiaji wa Sri Lanka waliokamatwa baharini

Picha@UNHCR/A. Di Loreto(UN News Centre)

Australia kuwafukuza wahamiaji wa Sri Lanka waliokamatwa baharini

Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi UNHCR limeeleza wasiwasi wake kuhusu maamuzi ya Australia kufukuza waomba hifadhi salama 41 kutoka Sri Lanka.  Mahakama Kuu ya Australia imesitisha pia maombi mengine 153 ya waomba hifadhi salama kutoka Sri Lanka.

UNHCR imesema, imepata taarifa kutoka mamlaka za Australia kwamba vigezo vya kuthibitisha maombi ya hifadhi vimeongezeka, ikisema pia shirika hilo limeshaielezea Australia kwamba sheria zake kuhusu kuwapatia watu hifadhi hazikubaliki na sheria za kimataifa.

Mkataba wa Wakimbizi wa 1951 unakataza kurejesha kwa nguvu watu ambao wameomba hifadhi.

UNHCR imeongeza, mtu yeyote ambaye anaomba hifadhi ana haki ya kusikilizwa kwa kesi yake ipasavyo kabla kurejeshwa kwao kama maombi yake hayakuthibitishwa.