Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Bokova asikitishwa na kifo cha Singh

Bokova asikitishwa na kifo cha Singh

Mkurugenzi Mkuu wa UNESCO, Irina Bokova, ameelezea kusitikitishwa kwake kutokana na kifo cha Balozi mwema wa UNESCO Madanjeet Singh kilichotekea tarehe sita Januari.

Amesema marehemu Singh alikuwa na juhudi na alijitolea katika kazi ya kuendeleza maelewano na amani na ni mfano wa kuigwa kwa watu kutoka mataifa, tamaduni na dini mbalimbali.

Ameongeza kuwa UNESCO imepoteza rafiki na msaidizi wa kweli. Katika kumulika kazi yake bora ya muda mrefu kwa ajili ya amani na maelewano, bodi ya UNESCO ilianzisha mwaka 1995 tuzo ya Madanjeet Singh kwa lengo la kuhamasisha kuvumiliana na kutokuwa na ghasia.

Singh aliteuliwa kuwa Balozi mwema wa UNESCO November 2000.