Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNEP yaanzisha mpango wa uzalishaji na utumiaji endelevu

Upandaji miti sahihi kwenye eneo husika hulinda mazingira halisi ya eneo hilo.@UNEP

UNEP yaanzisha mpango wa uzalishaji na utumiaji endelevu

Mpango mpya wa kuwawezesha wanunuzi kufanya maamuzi wanayoelewa wakati wanaponunua bidhaa za matumizi umezinduliwa leo, ukilenga kuhakikisha matumizi bora ya rasilmali.

Mpango huo ambao umezinduliwa na Shirika la Mpango wa Mazingira, UNEP, utalenga kutoa maelezo kamili kwa wanunuzi kuhusu athari za kimazingira na kijamii za bidhaa wanazotumia, kama njia muhimu ya kuchochea mienendo endelevu zaidi ya uzalishaji na utumiaji wa bidhaa.

Mpango huo wa kutoa maelezo kwa wanunuzi, ni sehemu ya pili ya mkakati wa mipango ya utumiaji na uzalishaji endelevu, 10YFP, ambao uliidhinishwa na mkutano wa maendeleo endelevu wa Rio+20 mnamo mwaka 2012.

Mpango huo utaongozwa kwa pamoja na serikali za Ujerumani na Indonesia, pamoja na Shirika la Consumers International, ukisaidiwa na UNEP, ambayo kwenye makao yake kunapatikana sekritariati ya 10YFP.