Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Nchi nne zaridhia mkataba kuhusu kutokuwa na utaifa

@UNHCR/ S. Boness

Nchi nne zaridhia mkataba kuhusu kutokuwa na utaifa

Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na wakimbizi UNHCR kwa pamoja na Ofisi ya sheria ya Umoja wa Mataifa, leo wanakutana kwa shughuli maalumu mjini Geneva ambako pia nchi za Ubelgiji, Gambia, Georgia na Paraguay zitajitokeza na kuridhia mkataba wa Umoja wa Maitaifa kuhusu watu wanaokosa utaifa. Taarifa kamili na Amina Hassan

Taarifa ya Amina Hassan

Tukio hilo la leo linatajwa kuwa la aina yake likihusisha mataifa zaidi ya matatu kushirika kwenye hafla ya kuidhinisha mkataba mmoja.

Kujitokeza kwa nchi hizo kwenye mkabata huo wa mwaka 1954 sasa kunafanya nchi jumla zilizoridhia kufikia 82 hatua ambayo inaongeza ishara ya matumaini.

UNHCR imesema kuwa hatua hiyo ni muhimu kwa vile inadhihirisha kuwa namna mataifa duniani yanavyotambua haja ya kushirikiana kukabiliana na tatizo la watu kukosa utaifa, tatizo ambalo limekuwa likiwaandama mamilioni ya watu duniani.

Kwa hivi sasa UNHCR imekuwa ikiendesha kampeni kuhusiana na mikataba yake miwili ambayo inapangwa kuzinduliwa rasmi Septemba 15 mwaka huu. Mikataba hiyo ina lengo la kukabiliana na tatizo la watu kukosa utaifa wao.