Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baraza la Haki za Binadamu lakutana kuhusu ukeketaji wa wanawake

Baraza la Haki za Binadamu lakutana kuhusu ukeketaji wa wanawake

(Sauti ya Pillay)

"Ukatili dhidi ya wanawake ni namna moja wapo ya uhalifu na ubaguzi wa kijinsia. Ni hatia dhidi ya haki ya utu wa mwanadamu. Ni hatia dhidi ya uhuru wa utesaji na ukandamizaji."

Washiriki wa mjadala huo wamejaribu kubaini mikakati mipya na kumulika mifano ya kuiga katika vita dhidi ya mila hiyo potofu. Pillay ameonya kuwa isipoongezwa bidii, ukeketaji labda unaweza kuchukua hata miaka 60 kutokomezwa,

(Sauti ya Pillay)

“Miaka sitini ni muda mrefu kusubiri. Kuodoshwa kwa Ukatili dhidi ya wanake, kutaboresha jamii na kutaleta uhuru dhidi ya maumivu na ukatili huo. wasichana na wanawake watajiendeleza katika uboreshaji na utumiaji wa vipaji vyao. Wanawake watapiga hatua mbele kiuchumi, kisiasa na kijamii. Tunahimiza serikali na mashirika yote husika, kutoa kipaumbele kwa kutokomeza ukeketaji.”

Pillay amesisitiza haja ya juhudi za pamoja kwenye ngazi ya kitaifa na kimataifa ili kukabiliana na suala hili nyeti.