Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ushirikishaji watoto wasaidia kudhibiti Pepopunda

Muhudumu wa afya akitoa tiba dhidi ya Pepopunda. Picha@WHO

Ushirikishaji watoto wasaidia kudhibiti Pepopunda

Ugonjwa wa Pepopunda husababisha kifo iwapo tiba haitachukuliwa mapema, halikadhalika iwapo kinga itapuuzwa. Shirika la afya duniani linasema kuwa Pepopunda huambukizwa na bacteria Clostridium tetani aliyeenea kwenye mazingira na humuingia binadamu kupitia kidonda kilicho wazi. Nchini Kenya, hatua zinachukuliwa na watoto wanashirikishwa vyema ili kuwaepusha na ugonjwa huo hatari. Je ni hatua zipi, basi ungana na John Ronoh kwenye makala hii.