Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mwendesha Mashtaka wa ICC atoa chapisho la sera kuhusu halifu wa kingono na kijinsia

Mwendesha Mashtaka Mkuu wa ICC Fatou Bensouda. (Picha: Maktaba ya UM/Evan Schneider)

Mwendesha Mashtaka wa ICC atoa chapisho la sera kuhusu halifu wa kingono na kijinsia

Normal

0

false

false

false

MicrosoftInternetExplorer4

st1\:*{behavior:url(#ieooui) }

/* Style Definitions */

table.MsoNormalTable

{mso-style-name:"Table Normal";

mso-tstyle-rowband-size:0;

mso-tstyle-colband-size:0;

mso-style-noshow:yes;

mso-style-parent:"";

mso-padding-alt:0in 5.4pt 0in 5.4pt;

mso-para-margin:0in;

mso-para-margin-bottom:.0001pt;

mso-pagination:widow-orphan;

font-size:10.0pt;

font-family:"Times New Roman";

mso-ansi-language:#0400;

mso-fareast-language:#0400;

mso-bidi-language:#0400;}

Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu, ICC, Fatou Bensouda, leo ametoa chapisho la kisera kuhusu uhalifu wa kingono na ule unaohusu jinsia.

Chapisho hilo la kina litatumiwa kutoa mwongozo kwa Ofisi ya Mwendesha Mashtaka katika kazi yake ya kuhakikisha wanaotenda uhalifu wa kingono na wa kijinsia hawakwepi mkono wa sheria, pamoja na kuendeleza uwazi na matumaini katika kuutekeleza mfumo wa sheria wa Mkataba wa Roma, ambao uliiunda mahakama ya ICC.

Katika taarifa iliyotolewa na Ofisi yake, Mwedesha Mashtaka huyo amesema sera hiyo pia itachangia siyo tu kufanya uchunguzi yakinifu na ufunguaji mashtaka kwa uhalifu wa kingono na ule unaohusiana na jinsia, bali pia katika kupanua wigo wa utendaji wa haki kwa waathiriwa wa uhalifu huo, kupitia mahakama ya ICC.

Bi Bensouda amesema uhalifu wa kingono na kijinsia ni miongoni mwa makosa mabaya mno chini ya Mkataba wa Roma, na kuchunguza na kufungulia mashtaka uhalifu huo ni suala la kipaumbele kwa Ofisi ya Mwendesha Mashtaka wa ICC. Amesema chapisho hilo la sera linatoa msingi wa kutumiwa kuhakikisha kuwa uhalifu wa kingono na kijinsia unakabiliwa ipasavyo.