Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hatua zichukuliwe kulinda utofauti wa bayoanuai asilia ya misitu

Msitu: Picha ya Joshua Mmali

Hatua zichukuliwe kulinda utofauti wa bayoanuai asilia ya misitu

Normal

0

false

false

false

MicrosoftInternetExplorer4

/* Style Definitions */

table.MsoNormalTable

{mso-style-name:"Table Normal";

mso-tstyle-rowband-size:0;

mso-tstyle-colband-size:0;

mso-style-noshow:yes;

mso-style-parent:"";

mso-padding-alt:0in 5.4pt 0in 5.4pt;

mso-para-margin:0in;

mso-para-margin-bottom:.0001pt;

mso-pagination:widow-orphan;

font-size:10.0pt;

font-family:"Times New Roman";

mso-ansi-language:#0400;

mso-fareast-language:#0400;

mso-bidi-language:#0400;}

Shirika la Chakula na Kilimo, FAO limetoa wito kwa nchi kuboresha ukusanyanji wa maelezo na utafiti ili kuendeleza uhifadhi na udhibiti endelevu wa rasilmali za misitu ya dunia, ambazo zinazidi kukabiliwa na shinikizo kubwa.

Kulingana na chapisho la kwanza la ripoti kuhusu hali ya rasilmali asilia za misitu ya dunia, nusu ya aina za miti inayoripotiwa kutumiwa mara kwa mara na nchi inakabiliwa na tishio la kugeuzwa kwa maeneo ya misitu kuwa mashamba ya kulima na malisho ya mifugo, kutumiwa kiholela na athari za mabadiliko ya tabianchi.

Mkurugenzi Msaidizi wa idara ya misitu katika FAO, Eduardo Rojas-Briales, amesema misitu hutoa chakula, bidhaa na huduma ambazo ni muhimu kwa uhai na ubora wa maisha ya mwanadamu, akiongeza kuwa faida hizi zote zinategemea uhifadhi wa utajiri wa utofauti wa asili ya bayoanuai ya misitu, ambayo imo hatarini.  Ameongeza kuwa ripoti hiyo ni hatua kubwa katika kuongeza akiba ya habari na elimu inayohitajika ili kuchukua hatua ya uhifadhi bora zaidi na udhibiti endelevu wa rasilmali azizi za misitu.