Uharibifu wa mazingira wahatarisha ziwa Albert Uganda
Uhabribifu wa maliasili kama vile maziwa na mito huchangiwa na shughuli kadhaa za kibinadamu ambazo wakati mwingine huhalalishwa kwa sababu mbalimbali ikiwamo kujipatia kipato.
John Kibego kutoka Uganda anangazia athari za mazingira zitokanazo na uchimbaji mchanga kwenye ziwa Albert nchini humo.
Afrika haihiitaji msaada toka nje, bali usawa katika biashara: Rais wa Ghana
Rais John Dramani Mahama wa Ghana amehoji nini kilichoyakumba maadili yaliyoanzisha Umoja wa mataifa. Akizungumza katika mkjadala wa wazi wa baraza kuu Jumatano amesema hivi sasa duniani kote k kuna kuta mpya zinazojengwa ili kuwafungia watu, na hali hii itaendelea kwa muda gani?
Hali ya utulivu yarejea Kenya
Inayofuata ni mukhtasari wa ripoti kuhusu shughuli za UM nchini Kenya ikiwa miongoni mwa harakati za kurudisha utulivu na amani kwa umma kijumla baada ya machafuko ya karibuni.
Juhudi za UM kurudisha amani Kenya
Baraza la Usalama lilikutana Ijumatano jioni kushauriana juu ya udhibiti bora wa athari za machafuko yaliotukia Kenya hivi karibuni.
Baraza la Usalama kusikia fafanuzi za KM juu ya hali Kenya
Ijumanne, KM wa UM Ban Ki-moon aliripoti mbele ya Baraza la Usalama juu ya ziara aliyofanya majuzi Afrika ambapo alizungumzia misukosuko na vurugu liliofumka barani humo, hususan katika Chad na Kenya, na kushauriana juu ya namna ya kukidhi mahitaji ya msingi kwa waathiriwa wa vurugu.~~
UM wahudumia Misaada ya Kiutu na Kisiasa Kenya
Tumekuandalieni ripoti mbili zinazoelezea operesheni za mashirika ya UM yanayohusika na huduma za dharura za wahamiaji (UNHCR) na pia operesheni za kugawa miradi ya chakula duniani (WFP) kwa waathiriwa wa maafa.
Mchango wa Umoja wa Mataifa Kurudisha Amani Kenya
Hii leo tunaanza mfululizo wa vipindi maalumu, vya kila siku, vya dakika tano, kuhusu juhudi za UM kuisaidia Kenya kurudisha utulivu na amani nchini, na vile vile kuhudumia misaada ya kiutu kwa wale waathiriwa wa machafuko ya karibuni.