Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Idadi ya wakimbizi wa Sudan Kusini nchini Uganda yaongezeka:UNHCR

Wakimbizi wa Sudan Kusini wkiwa Dzaipi, moja ya vituo vya muda vya kuhifadhi wakimbizi huko Uganda. (Picha@UNHCR)

Idadi ya wakimbizi wa Sudan Kusini nchini Uganda yaongezeka:UNHCR

Mzozo unaoendelea huko Sudan Kusini unazidi kumiminisha wakimbizi kwenye nchi jirani ambapo Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi la (UNHCR) linasema mwezi Mei pekee wakimbizi zaidi ya Elfu Kumi waliingia Uganda. Kutoka Uganda John Kibego wa Radio washirika Spice FM anaripoti kamili.

(TARIFA YA JOHN KIBEGO)

Mgogoro unaohushisha bunduki ambao ulianza Disemba mwaka jana Sudan Kusini, unaendela kuwalazimisha raia wake kukimbilia hapa Uganda.

Ripoti ya UNHCR kuhusu hali ya wakimbizi ya Mei 31, inasema idadi ya wakimbizi wa Sudan Kusini ilipanda hadi 113,094 kutoka wakimbizi 102,807 kilingana na hesabu ya tarehe 30 mwezi April.

Wengi wao walieleza kukimbia makabiliano baina ya wasi wa aliyekuwa makamu rasi Riek Machar na jeshi la serikali ya Sudan Kusini katika majimbo ya Upper Nile na Jonglei.

Kwa sasa wanahifadhiwa katika makambi na vituo vya kupokea wakimbizi yakiwemo Nyumanzi, Dzaipi Paratuku na Kiryandongo.