Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Watu mashuhuri duniani wazindua video kuwaunga mkono wakimbizi

Msafiri Tawimbi amekimbia DRC mwaka 1996, alibaki na shati lake kukumbuka aliyoyapitia @UNHCR/M. Senelle

Watu mashuhuri duniani wazindua video kuwaunga mkono wakimbizi

Normal

0

false

false

false

MicrosoftInternetExplorer4

Watu mashuhuri duniani wamezindua video zinazohimiza haja ya kuendelea kuwaunga mkono wakimbizi ambao baadhi wanaishi maisha ya shida na taabu.

Nyota hao wanaofikia 20 wakiwemo mtunzi maarufu wa vitabu, Khaled Hosseini, mwigizaji wa Ujerumani Diane Kruger na mwanamziki wa  Colombian Juanes wamezindua video hizo zenye sekunde 30 kama sehemu ya kuelekea kilele cha siku ya wakimbizi duniani itakayoadhimishwa Juni 20 mwaka huu

Taarifa kamili na George Njogopa

Taarifa ya George

Wakati huu ambako kunashududiwa idadi ya mizozo ikiongezeka na kusababisha mamia ya raia kukimbia makazi yao, Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia wakimbizi UNHCR limeanza kufanya kazi na mabalozi wa hisani pamoja na watu wengine mashuhuri kuwapa maneno ya matumaini wakimbizi.

Kamishna wa UNHCR Antonio Guterres amesema kuwa dunia wakati huu inakabiliwa na changamoto kubwa ya kuwalinda na kuwasaidia mamia ya raia wanaoangukia maisha ya ukimbizi kutokana na machafuko yanayoendelea kila uchao katika maeneo mbalimbali.

Kamishna huyo ametambua kazi inayofanywa na watu hao mashuhuri ambao amesema wamejitokeza hadharani na kuelezea madhila wanayokumbana nayo wakimbizi , lakini wakati huo huo wakituma ujumbe wa matumaini kwao.

Video hizo ambazo zinaanza kupatikana leo kwenye mitandao mbalimbali, ni sehemu ya kampeni ya kuelimisha watu hasa wakati huu wa kuelekea kwenye kilele cha siku ya wakimbizi duniani inayoadhimishwa kila mwaka Juni 20.

st1\:*{behavior:url(#ieooui) }

/* Style Definitions */

table.MsoNormalTable

{mso-style-name:"Table Normal";

mso-tstyle-rowband-size:0;

mso-tstyle-colband-size:0;

mso-style-noshow:yes;

mso-style-parent:"";

mso-padding-alt:0in 5.4pt 0in 5.4pt;

mso-para-margin:0in;

mso-para-margin-bottom:.0001pt;

mso-pagination:widow-orphan;

font-size:10.0pt;

font-family:"Times New Roman";

mso-ansi-language:#0400;

mso-fareast-language:#0400;

mso-bidi-language:#0400;}